Ad Code

MAISHA YA DIKTETA ADOLF HITLER

historia na maisha ya wababe wa dunia

MAMBO USIYO YAFAHAMU KUMHUSU DIKTETA ADOLF HITLER

adolf Hitler

Wanahistoria Na Watu wengi Duniani wamekuwa wakisimulia kuhusu Maisha ya Dikteta Adolf Hitler Wa Ujerumani .Leo ndani ya nijuze bongo Ninamuelezea kwa kifupi Hitler kuwa ni nani ktk Historia ya Dunia Hii. Je ,Adolf Hitler alikuwa katili tu hakuwa na Mema ktk Maisha yake ? Fuatilia Historia hii .


Adolf Hitler alizaliwa Aprili 20, Mwaka 1889 ktk mji mdogo Wa Austria ujulikanao kama Braunau .Baba yake alikuwa anajulikana kwa jina la Alois Hitler ambaye baadaye alikuja kuwa Afisa Forodha Mkuu .Mama yake Adolf Hitler aliitwa Klara ambaye ni mtu aliyetokea katika familia masikini kabisa ya Kikulima . Adolf Hitler hakufanikiwa kusoma kwani aliamua kutoroka na kuacha shule mnamo mwaka 1905.Baadaye alitamani sana kusoma chuo cha Sanaa cha Vienna lakini alikataliwa . Historia inaonyesha kwamba Adolf Hitler akiwa shule ya Msingi alikuwa na uwezo mkubwa darasani na alikuwa mtu maarufu sana miongoni mwa wanafunzi wenzake huku sifa za kuwa kuwa kiongozi bora zikimbeba .


Ktk Elimu ya Serikali kulikuwa na ushindani mkubwa sana na hivyo Hitler aliamua kusimama kimasomo .Alisimama kimasomo akiwa na Umri mdogo sana Wa miaka 15 hivyo Elimu rasmi ikawa imemshinda .


Akiwa na Umri Wa takribani miaka 18 aliamua kwenda hadi mjini Vienna huku akiwa na fedha alizokuwa amerithi baada ya baba yake kufariki Dunia mnamo mwaka 1903,Alikwenda huko ili atafute nafasi ya masomo ktk chuo cha Sanaa cha Vienna na Chuo cha Ujenzi lakini kwa bahati alikataliwa kutokana na kukosa Sifa .Baada ya kushindwa kujiunga na vyuo hivyo Alipenda sana Siasa na kuanza kuzifuatilia kwa karibu ndipo ndoto za kuwa Kiongozi Wa Taifa la Ujerumani zilianza kumjia .


Historia inaonyesha Adolf Hitler ktk vita Ya kwanza ya Dunia alikuwa ni mpiganaji Wa kujitolea ktk jeshi la Ujerumani na hatimaye alipata nafasi ya UKopuro(copro) na baadaye alibahatika kupata zawadi ya mkimbiaji bora vitani na akapewa nafasi ya mjumbe wa mawasiliano jeshini .Hapo ndipo ilianza safari yake ya kupelekea uzoefu kamili jeshini na kuanza kuibukia ktk majukwaa na mikutano ya Kisiasa .Endelea kufuatilia bila kuchoka Historia hii fupi ya Dikteta huyu maarufu Duniani.


Adolf Hitler Aliibuka na kuwa miongoni mwa Madikteta wenye nguvu na umaarufu mkubwa sana Duniani ktk karne ya 20.Baada ya vita vya kwanza vya Dunia Adolf Hitler aliibuka na kuwa kiongozi mkuu Wa Serikali Ya Ujerumani kupitia chama cha National Socialist German Workers Party mnamo mwaka 1933.Kupitia kuanzisha kwake kwa makambi ya Mauaji pamoja na mateso dhidi ya watu wasiokuwa Wajerumani hasahasa akiwalenga na kuwaua Wayahudi Takribani 6000000(Milioni sita) kulimfanya aonekane kuwa ni mbaguzi Wa Rangi .Haya yalikuwa ni Mauaji ya Halaiki yasiyoweza kusahaulika ktk Historia ya Dunia.


Jitihada na chokochoko zake zilisabanisha kuivamia kijeshi nchi ya Poland mnamo 1939 na Hatimaye vita ya pili ya Dunia ilitokea .Hadi mwaka 1941 Ujerumani ilikuwa inashikilia sehemu kubwa ya Kaskazini mwa Afrika .


Kabla ya kuwa Kiongozi Wa Taifa la Ujerumani Historia inaoonyesha alikuwa ni mwanajeshi Wa kawaida kabisa jeshini .Kuna muda Aliwahi Toroka mafunzo ya kijeshi jeshini huko Austria -Hungary mnamo mwaka 1913 lakini alirudishwa kwa nguvu.Baada ya muda alianza tena kujitolea ktk jeshi la Balvaria na hatimaye mwaka 1914 alingia vitani huku akiwa askari Wa Kikosi kilichokuwa mstari Wa mbele upande Wa magharibi mwa nchi.Mwaka 1918 Hitler alipata ulemavu wa macho baada ya Gesi kumpata usoni .Wakati majeshi ya Ujerumani ikisalimu Amri Hitler alikuwa yupo Hospitalini na Aliporudi Nchini Ujerumani alikuta Uchumi umeyumba vibaya huku Wajerumani wakikosa matumaini kabisa .Uzoefu alioupata ktk mapigano ulimuathiri sana vibaya kiwango cha muda mwingi ktk maisha yake alikuwa akiwaza na kupenda vita .


Mwaka 1919 Adolf Hitler aliudhuria mkutano Wa kwanza Wa chama cha kijamaa cha Wafanyakazi na mkutano wa Kundi la wazarendo Wa Ujerumani ,Ktk mikutano hii Hitler aliudhuria kama jasusi Wa Jeshi.Baadaye alijikuta akikubaliana na Mawazo ya Anton Dlexler ambayo yalikuwa yakisisitiza Utaifa na Kupinga maonevu lakini hakukubaliana kwa namna ambavyo walikuwa wamejipanga kuyatekeleza Mawazo yao.Katika mkutano huo Adolf Hitler aliinuka na kupewa nafasi kisha kuanza kutoka hotuba iliyokuwa imejaa Upole na ukali ndani yake .Ktk Hotuba yake Hitler alieleza jinsi gani mkataba Wa Versailles ulivyokuwa unaiumiza nchi ya Ujerumani .


Ilifahamika wazi kuwa watu Wengi walianza kujiunga na chama hicho ili kumfuata Hitler na kusikiliza hotuba zake ambazo zilijaa ushawishi ,Elimu na Hamasa kubwa kwa Wajerumani wengi .Wajerumani baada ya kusikiliza hotuba zake walikuwa wapo Tayari kufanya jambo lolote ikiwa wangeamriwa.


Ikumbukwe Adolf Hitler baada ya vita vya kwanza vya Dunia alibaki hana kazi yeyote .Huu ndio ulikuwa muda wake Muafaka Wa kutekeleza ndoto na Malengo yake kwa Taifa la Ujerumani.Akiwa Mitaani na wanajeshi wenzake waliokuwa wamerejea kutoka vitani lakinihawana kazi waliendelea na harakati zao za mapambano kwenye mitaa ya Ujerumani.Mwaka 1919 alibahatika kupata ajira mjini Munich inasadikika alikuwa na mahusiano mazuri na Ofisa mmoja Wa Kijeshi ajulikanaye kwa Jina la Ernst Roehm .Baadaye Hitler akawa mwanapropaganda mzuri jeshini na kuanza kwa nguvu kujihusisha na chama cha Wafanyakazi cha kijerumani .


Mnamo Septemba 1919 Adolf Hitler alianza kushiriki mikutano kibao ya Chama cha Wafanyakazi .Ktk mikutano hiyo alikuwa ni mzungumzaji Mwenye ushawishi mkubwa kutokana na propaganda zake .Hitler alikuwa ni bingwa Wa kujenga hoja ktk chama cha KiNAZI.Hoja za Hitler zilijikita zaidi ktk kuupigania Utaifa na kuchochea zaidi Ubaguzi Wa Rangi .Aliongeza sana ushawishi kwa watu na maelfu ya wanachama walijiunga na chama cha National Socialist German Workers Party (NSDAP) jina rasmi chama cha NAZI .


Kutokana na Hali ngumu ya Uchumi miaka iliyofuata ilichangia kwa Kiwango kikubwa kukua kwa chama hicho .Hadi Mwishoni mwa mwaka 1923 idadi ya wanachama Wa chama cha NAZI walikuwa wamefikia 56000 hao ni yeye tu aliokuwa amewaongeza Ktk chama chake akawa maarufu sana ktk jeshi la Balvaria na Siasa za Ujerumani.Hitler alitumaini kuwa angetumia Udhaifu Wa Hali ngumu ya Kiuchumi kuipindua Serikali ya Mjini Berlin.Kwa dhamira ya dhati kabisa ya Kuipindua Serikali alianzisha maandamano na Fujo mnamo Novemba 8-9-1923 huku akitumaini kabisa kuwa Serikali ya Ushirika ya Balvaria ingeshirikiana naye kuipindua Serikali ya Berlin .Jaribio hili la kuipindua Serikali Ya Berlin lilishindikana.Najua una shauku kubwa kujua nini Kilifuata ,,Usichoke kufuatilia.


Baada ya jaribio hili la mapinduzi Adolf Hitler alishitakiwa kwa Makosa ya Uhaini dhidi ya Serikali ya Ujerumani kisha akahukumiwa kifungo Cha Kwenda Gerezani ktk Mji Wa Ngome Ya Zamani ya Landsberg .Kipindi ambacho Adolf Hitler yupo Gerezani Mawazo yake Ya mikakati na mbinu yalikua kwa kiwango kikubwa sana Nchini Ujerumani.Adolf Hitler alifanikiwa kuandika kitabu chake kijulikanacho kama MEIN KAMPF ktk kitabu hicho ali orodhesha Mipango na Imani .Adolf Hitler alifanikisha kuandikwa kwa kitabu chake hicho kwa kumtajia maneno na kisha kuandika mwandishi mmoja aliyemuamini sana ajulikanaye kwa jina la RUDOF HESS ambaye aliishi kati ya mwaka 1894 -1987 . Mipango na Imani hizo zililenga hasa ktk Kukiunda upya chama cha Kijamaa na Wafanyakazi .Mara kadhaa Akiwa Gerezani alifanya jitihada nyingi zilizolenga kukata rufaa dhidi ya Hukumu ya kifungo Gerezani.


Baadaye Hitler aliachiwa Huru ,Mara baada ya kuachiwa huru alizirejea Siasa zake kisha kuanza kurejesha ushawishi wake ktk chama cha NAZI .


Baada ya mapinduzi ya Serikali kushindwa mnamo mwaka 1923 alikamatwa na kutiwa jela ambapo baada ya Kutoka jela aliendelea kukijenga chama chake ili kije kishike madaraka kwa njia ya Kisheria (Legal means) .


Aliamini kuna majira yangekuja angeanza kuijenga ujerumani mpya kwa misingi ya Rangi (Ubaguzi Wa rangi) ambapo angeongeza ukubwa Wa Ujerumani kwa kuvamia na kutawala maeneo mbalimbali Ya Dunia.


Aliamini Kwamba Ujerumani ni lazima ipigane vita vingi ili ikalie Eneo kubwa la Ardhi na Wajerumani waendeshe shughuli mbalimbali za Kilimo na viwanda .Vita ndogo na rahisi ilipiganwa dhidi ya nchi ya Czechoslovakia ,ikifuatiwa na vita kubwa dhidi ya Ufaransa na Uingereza na vita ya Tatu ambayo ingefuata ambayo ilitegemewa ingekuwa rahisi na haraka ni zidi ya Muungano Wa Jumuiya ya Kisovieti (Urusi) ambapo Ujerumani ingepata malighafi nyingi Hususani mafuta na Vita ya Nne na ya mwisho iliyopangwa na Adolf Hitler ilikuwa ni dhidi ya Taifa la Marekani.


Mipango hii ya vita ingeweza kufanikiwa ikiwa Ujerumani ungekuwa na Ndege vita na Meli za kivita zenye Uwezo Wa kushambulia kwa masafa

.

Safari yake ya kuingia Serikalini na kutimiza azima na mipango ya Kuiteka Dunia iliendelea kubaki kichwani mwake .Miaka ya 1930 Dunia ikiwa katika Mvurugiko Wa Kiuchumi Adolf Hitler alianza kushamiri na kuwa mtu maarufu Sana ktk Siasa Za Ujerumani kama ambavyo awali nimeelezea .Katika Uchaguzi Wa Septemba 1930 Chama cha NAZI kilipata takribani Kura 6500000 Hatimaye kuwa na Umaarufu usio na shaka ktk Siasa za Ujerumani.Mwezi Novemba 1932 Rais Wa Ujerumani mh.Paul Von Hindenburg aliyeishi kuanzia mwaka 1847-1934 alimuita Adolf Hitler kisha kumfanya Awe Kansela ili kuiongoza Serikali Ya Muungano ya KiNAZI ,Watu wazalendo na watu mbalimbali huru na maarufu .


Kwa miaka miwili ya Mwanzo Adolf Hitler alionyesha heshima kubwa ktk kutoingilia mihimili mingine Yaani Mahakama na Bunge .Kutokana na wadhifa muhimu ktk Serikali ya Kijeshi ya chama cha NAZI ,Hitler alianza kumtumia aliyekuwa Rafiki yake na waziri wa Ulinzi ambaye alijulikana kwa Jina la Werner Von Blomberg ,Taratibu Hitler alianza kuiongoza Wizara hiyo .Adolf Hitler alianza kuwaondoa mahasimu wake Wa Kisiasa huku Akihakikisha Ngazi zote za kiserikali na Taasisi kuu Za Kisiasa zipo chini ya Udhibiti wake .Kufuatia kifo cha Rais Hindenburg Mwezi Oktoba 1934 basi ikawa ndio Yake rahisi ya Kufuta cheo cha Urais ,Hatimaye rasmi Adolf Hitler akawa Kiongozi Mkuu Wa Serikali ya Ujerumani na Amiri Jeshi Mkuu Wa Majeshi ya Ujerumani .Baada ya Muda alimteua Joseph Goebells kuwa Mkuu Wa kitengo cha propaganda aliyezaliwa mwaka 1887 na kufariki Dunia mwaka 1945 pia alimteua Heinrich Himmler kuwa Mkuu Wa Polisi Wa Ujerumani .Utawala Wa Adolf Hitler ulionekana kuwa na mvuto mkubwa baada ya mamilioni ya Watu Wa Ujerumani kuandamana huku wakimshangilia mnamo mwaka 1934 .


Baada ya kuhakikisha nchi ya Ujerumani imedhibitiwa vilivyo alianza kuhamasisha maliasili za Wajerumani zitumike kwa ajili ya uvamizi ktk mataifa jirani na Kuhakikisha Ubaguzi Wa Rangi unatawala Upande wa katikati na Mashariki mwa Ulaya .Aliwaandaa watu waliokuwa hawana kazi takribani 6000000 ili wafanye kazi kwa ajili ya maandalizi ya Vita .Kutokana na propaganda za kikatili Hitler aliwaua wayahudi wengi ambapo alidai wao ni sababu ya matatizo ya Ndani na nje ya Ujerumani.Kitu kinachoogopesha na kutisha ni kwamba Hitler alitoa amri wayahudi waliokuwa watoto ,wanaume na wanawake wachomwe moto kwenye matanuri yaliyokuwa yameandaliwa kwenye makambi maalumu yaliyokuwa chini ya udhibiti Wa Himmler .Mahusiano ya kigeni zaidi yalijikita ktk maandalizi ya vita .Kutokana na Jeshi la Ujerumani kuboreshwa na kuwa na nguvu pia kupata washirika Wa mataifa mengine ndio Ikawa hatua muhimu sana ya maandalizi ya vita kama vilivyokuwa ndoto zake tangu mwanzo yaani kuiteka Ulaya na Dunia yote .Hitler alivamia na kudhibiti Czechoslovakia ,Austria mnamo mwaka 1939 .Hatimaye ,kupitia ahadi na vitisho chake alianza kujipenyeza na kutaka kuvamia Uliokuwa Muungano Wa Kisovieti ambao ulikuwa ukiundwa na Urusi na vinchi vidogovidogo . Ujerumani ilipata Muungano Wa Kijeshi Wa Taifa la Japan na Italia .Muungano huu ulikuwa muhimu sana kuelekea maandalizi ya Vita.


Mnamo Septemba 1,1939 Adolf Hitler alianzisha vita Ya Pili ya Dunia kwa kuivamia kijeshi nchi ya Poland lengo lake hasa aitawale Ulaya Yote .Uvamizi huu Wa ghafla dhidi ya Poland ulienda sambamba na maangamizi makubwa ya Wayahudi wakati huo na wasomi wengi Wa Poland waliuawa vibaya na hatimaye Eneo la Poland Likawa chini ya Utawala Wa Kikoloni Wa Kijerumani.


Baada ya Uvamizi huo Wa Adolf Hitler Uingereza na Ufaransa walitangaza vita zidi ya Ujerumani. Mara tu baada ya tangazo hili la Vita majeshi ya Hitler yaligeuzia Silaha za kivita upande Wa magharibi mwa Ulaya na Hatimaye kuvamia na kuua vibaya pamoja na kuleta athari mbalimbali.Baada ya mashambulizi makali mnamo Aprili 1940 Nchi ya Denmark ilijisalimisha kwa Ujerumani na baadaye nchi ya Norway ilifuatia .Mwezi Mei na Juni Majeshi ya Hitler yalisonga mbele huku yakiwa yamejihami vilivyo kwa Vifaru na Ndege za kivita hatimaye nchi ya Ufaransa na nchi nyingine ndogondogo zilizopo karibu Zilipigwa Vibaya .


Kutokana na Uimara Wa jeshi la Anga la Uingereza na Ufaransa, majeshi ya Ujerumani yaliondolewa kwa nguvu na Hatimaye Hitler aliamuru kurudishwa nyuma jeshi lake ili lijipange vizuri zaidi .


Mengi kubwa la Hitler lilikuwa ni Kuvamia Eneo lote la Mashariki ili kurahisisha harakati zake za Kuiteka Ulaya .Mnamo Juni 22,1941 jeshi la Ujerumani lilisonga mbele zaidi ktk Operesheni yake ijulikanayo kama BARBARROSSA ,Ambayo Hitler alidai kwamba hii Ni Opesheni ya Harakati za Mwisho za Kuendelea kuishi na Kuwepo ktk Dunia .Ingawaje majeshi ya Adolf Hitler yalisonga mbele kwa haraka sana lakini hayakufanikiwa kutimiza malengo makuu Matatu kwani Majeshi ya Urusi yaliwazuia kusonga mbele zaidi .Malengo makuu matatu ya majeshi ya Hitler yalikuwa ni kufikia Miji mikubwa mitatu ambayo ni :MOSCOW,LENINGRAD na STALINGRAD .Miaka iliyofuata Nguvu ya jeshi la Adolf Hitler ilizidi kushuka Tofauti na matarajio na kikwazo kikubwa ilikuwa ni namna ya Kuvamia na kuchukua mji Wa STALINGRAD mwaka 1943 .Mwaka uliofuata majeshi ya Muungano Wa Uingereza, Marekani, Ufaransa na Urusi yaliendelea kusonga mbele mpaka ndani ya Makao Makuu Ya Serikali ya chama cha NAZI iliyokuwa chini ya Dikteta Adolf Hitler.

.

Itaendelea katika chapisho lingine............

Post a Comment

0 Comments